MAJALIWA: RAIS SAMIA AMETOA SH. BILIONI 50 ZA KUNUNUA MAHINDI

* Yatanunuliwa kuanzia Jumatatu Septemba 13, 2021 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa sh. bilioni 50 ambazo zitatumika kununua mahindi kutoka kwa wakulima ili kuwanusuru na kudodora kwa bei ya zao hilo. Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Septemba 10, 2021) Bungeni wakati akiahirisha mkutano wa nne wa Bunge la 12,